BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
SHIRIKISHO la soka chini (TFF) limetolea ufafanuzi kuhusu suala la beki Hassan Kessy kucheza kwenye mchezo wa jana uliomaliza kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toto African na kusema alikuwa sahihi kwani hoja ya Simba ni kwamba mchezaji huyo alivunja mkataba baada ya kusaini kwa mabingwa hao huku akiwa bado na Mkataba na vinara wa ligi na sio pingamizi ya usajili.

Akizungumza na waandishi wa habari, Afsa habari wa Shirikisho hilo Alfred Lucas aliema; "Kuna minong'ono kuwa Yanga watakatwa pointi kwa kumchezesha Kessy hiyo habari sio kweli, Simba inadai beki huyo alivunja mkataba ila hawakuweka pingamizi kwenye usajili wake kwahiyo ni sahihi kuendelea kuwatumikia mabingwa hao huku suala lake likiendelea kushughulikiwa."

Kwa mujibu wa mkataba wa Simba na beki huyo, Kessy anatakiwa kuilipa Simba dola 600,000 kwa kuvunja mkataba ambapo TFF limezitaka pande zote kukutana haraka kumaliza suala hilo.

Post a Comment

 
Top