BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma,Dar
HALI ya usalama katika uwanja wa Taifa umeimarishwa kuelekea mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga ambao utafanyika masaa machache yajayo.

Vikosi mbalimbali vya ulinzi vya Jeshi la Polisi vinafanya doria kuzunguka uwanja mzima kulinda usalama wa raia na mali zao.


Idadi hiyo ya askari inaenda sambamba na mashabiki wanaoendelea kuingia uwanjani kulingana na ukubwa wa mechi yenyewe ambayo inavuta  hisia za wengi.

BOIPLUS imezunguka kila mahala uwanjani hapa lakini hakuna tukio lolote la uvunjifu wa amani lililojitokeza hadi sasa licha ya misururu mirefu ya kuingia uwanjani.

Post a Comment

 
Top