BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Dar
NYOTA watatu wa Maafande wa JKT Ruvu wamerejea kikosini kuongeza nguvu kuelekea mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar mtanange utakaopigwa kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.

Nyota hao ni Hassan Dilunga, Michael Aidan pamoja na Emmanuel Pius huku beki Nurdin Mohamed akiendelea kuwa nje ya uwanja baada ya Afya yake kutotengemaa vizuri.

Msemaji wa Maafande hao Afisa Mteule daraja la Pili Constantine Masanja ameiambia BOIPLUS kuwa kikosi chao kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Mbweni JKT kuwavutia kasi 'Wakata miwa' hao wa Manungu Turiani.

"Kikosi kinaendelea vyema na mazoezi katika uwanja wa Mbweni tayari kwa mchezo wetu wa Jumamosi dhidi ya Mtibwa," alisema Masanja.

Masanja alisema benchi la ufundi la timu hiyo linatoa mafunzo maalumu kwa washambuliaji wao baada ya kukosa magoli mengi kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba wikiendi iliyopita.

"Tulipoteza nafasi nyingi kwenye mchezo dhidi ya Mbao, safu ya ushambuliaji ilikuwa butu walimu wameliona hilo na wamesema watalifanyia kazi," alisema Masanja.

Post a Comment

 
Top