BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu, Dar
NAIBU waziri wa Ardhi Nyumba na  Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula ambaye alikuwepo leo katika Uwanja wa Uhuru akishuhudia timu ya Mbao FC ya jijini Mwanza ikilala kwa mabao 3-0 amesema uchovu wa safari ndiyo sababu pekee ya timu hiyo kupokea kichapo.

Naibu Waziri huyo amekuwa akitoa msaada mkubwa kwa  kununua  vifaa mbalimbali  ili kuisaidia  timu hiyo iliyopo katika Jimbo lake la Ilemela  kufanya vizuri katika mechi za ligi kuhakikisha inawanyamazisha watu wanaoiponda kuwa ilipanda daraja kupitia mlango wa uwani. 


Mabula alisema kuwa  kilichowafanya washindwe kuwafunga Yanga ni uchovu wa safari tu hali iliyopelekea Mabingwa hao wawe kwenye kiwango bora kiasi cha Mbao kushindwa kuhimili kashkashi za vijana hao wa Jangwani.

"Mpira ni mchezo wa makosa, vijana wangu wamejituma na kupambana kwahiyo hatuwezi kukata tamaa, leo tulikuwa na uchovu wa safari na tumekutana na timu bora, tunaangalia michezo yetu ya mbele ili kuhakikisha tunakuwa katika nafasi nzuri  kabla ya mzunguko wa  kwanza haujamalizika," alisema Mabula.

Matokeo ya leo yameipeleka Mbao katika nafasi 11 wakiwa na alama 13 baada ya kushuka dimbani mara  13.

Post a Comment

 
Top