BOIPLUS SPORTS BLOG

MADRID, Hispania
MABINGWA watetezi wa ligi ya Mabingwa barani Ulaya timu ya Real Madrid imeibuka na ushindi mabao 5-1 dhidi ya Legia Warszawa ya Poland kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.

Gareth Bale aliwapatia goli la uongozi wenyeji dakika ya 16 kabla ya Tomasz Jodlowiec kujifunga akiwa kwenye harakati za kuokoa ambapo Miloslav Radovic aliwafungia wenyeji bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penalti.

Marco Asensio alifunga bao la tatu dakika ya 37 kabla ya Lucas Vasquez na Alvaro Moratta kufunga pazia la mabao kwa Madrid ambao waliwazidi sana Wapoland hao.

Matokeo mengine
Bayern Liverkusen 0-0 Tottenham Hotspur
CSKA Moscow 1-1 As Monaco
Sporting CP 1-2 Borrusia Dortmund
Club Brugge 1-2 FC Porto
Leicester City 1-0 FC Koebenhavn
Dynamo Zegreb 0-1 Sevilla
Olympic Lyon 0-1 Juventus

Post a Comment

 
Top