BOIPLUS SPORTS BLOG

BARCELONA, Hispania
PEP Guardiola ameshindwa kufanya vyema kwenye uwanja na Nou Camp baada ya kikosi chake cha Manchester City kukubali kichapo cha mabao 4-0 toka kwa Barcelona.

Lionel Messi alikuwa mwiba mchungu kwa City baada ya kufunga mabao matatu pekee yake 'hat trick' huku Neymar akimalizia la mwisho na kumfanya Guardiola atoke kichwa chini.


City walimaliza mechi hiyo wakiwa pungufu baada ya golikipa wao Claudio Bravo kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 53 kutokana na kudaka mpira nje ya eneo lake.

Hii ni mechi ya kwanza kwa Guardiola kurudi Nou Camp tangu alipoondoka mwaka 2014 na wamempokea kwa kichapo cha mabao manne.

Arsenal nao waliwafunga Ludogorets mabao 6-0 huku kiungo Mesut Ozil akifunga nae 'hat trick' na kuwafanya Washika bunduki hao kuwa kwenye nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora.

Matokeo mengine ni kama ifuatavyo
PSG 3-0 Basel
Dynamo Kiev 0-2 Benfica
Napoli 2-3 Bekistas
Celtic 0-2 Borussia Monch'bach
Bayern Munich 4-1 PSV
FC Rostov 0-1 Atletico Madrid

Post a Comment

 
Top