BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar
LICHA ya kuwa nyuma kwa alama sita dhidi ya vinara Simba mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga hawajayumba na wana imani watairejesha nafasi yao kabla ya kutawazwa mabingwa wa msimu wa 2016/17.

Baada ya sare ya Jumamosi dhidi ya Simba mabingwa hao wamerudi hadi nafasi ya nne kutokana na kufikisha alama 11 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi ambao watacheza na Maafande wa JKT Ruvu.

Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi alisema kuwa kwa sasa ni mapema mno kuwatoa kwenye kinyang'anyiro cha ubingwa kwakua wamecheza mechi tano pekee huku wakisalia na michezo mingine 25 kabla ligi kumalizika.

"Itakuwa ni maajabu leo hii kusema kuwa tumetolewa kwenye mbio za ubingwa, hata msimu uliopita kuna kipindi wenzetu waliongoza tena kwa muda mrefu lakini kilichotokea sisi ndiyo tuliibuka mabingwa," alisema Mwambusi.

Aidha kocha huyo wa zamani wa Mbeya City alisema wameweka mkazo zaidi katika mechi zao za nyumbani kwakua viwanja vya mikoani vingi havina ubora huku nyota wao wakikamiwa na wapinzani wao.

Endapo mabingwa hao watashinda mchezo wao wa kiporo dhidi ya Maafande hao watafikisha pointi 14 alama tatu pungufu ya vinara Simba ambao wana pointi 17 mpaka sasa.

Ligi imesimama kupisha michezo ya kirafiki ya kimataifa ambapo Octoba 8 timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itashuka dimbani ugenini kucheza na Ethiopia.

Post a Comment

 
Top