BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
YANGA ina pointi 24 ikiwa mbele ya Stand United kwa pointi tatu kwani wao wana pointi 21 na timu zote zinacheza leo Jumapili ila Wapiga Debe hao wanaomba Yanga ipoteze dhidi ya Mbao FC ili wao washinde na kuwafikia.

Yanga watakuwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakati Stand United wao wapo Uwanja wa Mabatini, Pwani kucheza na Ruvu Shooting. Mechi zote zinaonyesha kuwa na upinzani mkubwa kwani Yanga wanaifukuzia Simba iliyopo kileleni ikiwa na pointi 32 baada ya kushinda jana Jumamosi bao 3-0 dhidi ya Mwadui FC.

Hata hivyo, Yanga wakipoteza na Stand wakashinda timu zote zitakuwa na pointi sawa na Yanga ataendelea kukaa nafasi ya pili kwani ana tofauti kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa (19) tofauti na Stand ila watakuwa kwenye vita kubwa kushinda mechi zijazo ili mmoja apande nafasi ya pili huku Simba wao wakiwa bado wametulia kileleni.

Kocha wa Stand United, Athuman Bilali ameiambia BOIPLUS kuwa wanaangalia pointi za Yanga pale juu huku wakitafuta jinsi gani wataweza kufukuzana nao ili nao wajikite kwenye nafasi ya pili kama siku chache zilizopita kabla hawajashushwa na Prisons walipopoteza mechi hiyo huku Yanga wakipanda baada ya kushinda mechi zao za nyuma.

"Sasa hivi nataka nicheze kwa historia, nakumbuka kuna mwaka kabla Ruvu hawajashuka nilikuja hapa Mabatini niliwafunga Ruvu halafu nikarudi Shinyanga nikawafunga bao moja Simba, hivi ndivyo itakavyokuwa safari hii, hii ligi msimu hii ni ngumu sana kila timu inataka ushindi kwa njia yoyote ile.

"Jioni tunashinda hapa halafu hesabu zetu tunaenda kukamilisha na Simba ila jambo kubwa tunaloomba Mbao wawasimamishe Yanga maana ndiyo tunakimbizana nao. Simba jana wameifunga Mwadui kwasababu ya mapungufu yao ambayo sisi hatuna," alisema Bilal na kuongeza

"Mwadui hawakujipanga ndiyo maana wamepoteza mechi kirahisi hivyo tunamaliza hapa tutarudi nyumbani. Ni kweli Simba wametufunga msimu uliopita ambao ulikuwa wa Patrick Liewig na sio mimi," alisema.

Post a Comment

 
Top