BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
BEKI wa kati wa timu ya Yanga Kelvin Yondani ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake jioni ya leo kujiwinda na mchezo dhidi ya Mbao FC Jumapili akisumbuliwa na maambukizi ya fangasi vidoleni hali inayomsababishia maumivu.

Mabingwa hao walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam chini ya Kocha msaidizi Juma Mwambusi huku beki huyo kisiki akiwa pembeni kuwatazama wenzake kutokana na maagizo kutoka kwa Daktari wa timu hiyo.

Daktari Edward Bavu aliambia BOIPLUS kuwa beki huyo anasumbuliwa na fangasi miguuni na amemuaru kuvaa viatu vya wazi kwa ajili ya kupata hewa lakini anatarajiwa kuanza mazoezi na wenzake kesho ambapo Kocha kama ataona inafaa kumtumia Jumapili kwenye mchezo dhidi ya Mbao uwanjani hapo anaweza kucheza.


"Anasumbulia na fangasi lakini kesho ataanza mazoezi na wenzie kuna dawa anatumia na mwalimu akiona inafaa atamtumia kwenye mchezo dhidi ya Mbao," alisema Bavu.

Mbali na Yondani wachezaji wengine Nadir Haroub 'Canavaro' na Malimi Basungu na hawakuwepo mazoezini kutokana na sababu mbali mbali ambapo nahodha Canavaro alikuwa na matatizo ya Kifamilia.

Meneja wa timu hiyo Hafidh Saleh alisema kuwa Canavaro ana matatizo ya kifamilia huku Busungu akiwa hana taarifa yake ya kutofika mazoezini tangu Oktoba mosi kwenye mchezo dhidi ya Simba.

Post a Comment

 
Top