BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar
KOCHA msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi bado anaitambua ajira yake ndani ya klabu hiyo japokuwa kuna tetesi za kufanyika kwa mabadiliko ya benchi la ufundi muda wowote kianzia sasa.

Yanga inataka kufanya mabadiliko hayo baada ya uongozi kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao ambayo inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 11. Matokeo yanayodaiwa kuwaweka katika wakati mgumu wa kutetea ubingwa wao wa ligi.

Licha ya Yanga kukanusha lakini taarifa za uhakika ni kwamba Yanga wapo katika mazungumzo na kocha wa Zesco ya Zambia, George Lwandamina na kwamba Boniface Mkwasa anayeifundisha Taifa Stars atakuwa msaidizi wa Mzambia huyo.

Akizungumza na BOIPLUS, Mwambusi alisema hana habari na hayo ya kuletwa kocha mpya, anachokipigania kwa sasa ni kupata matokeo mazuri katika mechi zao zijazo ikiwemo ya Mtibwa Sugar aliyoilezea kuwa itakuwa ngumu kwani wapinzani wao wamepata matokeo mazuri.

"Hatujapata matokeo mazuri katika mechi zetu zilizopita, ila naamini  vijana wetu watajituma ili kurudisha imani kwa mashabiki ambao watajitokeza kushuhudia mechi hiyo," alisema Mwambusi.

BOIPLUS inafahamu kuwa Mwambusi yupo ndani ya mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa miaka miwili na Yanga aliosaini akitokea Mbeya City wakati Hans Pluijm yeye amefanikiwa kuipatia Yanga mataji mawili ya ligi kuu na kwamba mkataba wake ukivunjwa basi atalazimika kulipwa mshahara wa mwezi mmoja.

Post a Comment

 
Top