BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu, Dar
VIWANGO bora vya viungo wapya wa  Simba, Mzamiru Yassin na Mohamed Ibrahim ndivyi vinavyompa presha kubwa Awadh Juma anayecheza nafasi hiyo huku tayari viungo hao wakijihakikishia namba kwenye kikosi cha Joseph Omog.

Awadh hajacheza mechi hata moja msimu huu kwenye mzunguko wa kwanza uliomalizika wiki iliyopita kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti ingawa kwasasa amepona.


Simba iliwasajili viungo hao kutoka Mtibwa Sugar pamoja na winga Shiza Kichuya anayeongoza kwa kupachika mabao akiwa ametupia bao tisa ambapo Omog amekuwa akiwaamini na kuwatumia karibu kila mechi hali ambayo imeonyesha kumpa hofu Awadh kuhusu changamoto hiyo ya kupigania namba.

Mzamiru pia ameisaidia Simba kukusanya pointi 35 zilizowaweka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom akifunga mabao manne huku Ibrahim akitupia bao mawili.

Awadh ameiambia BOIPLUS kuwa "bado nina uwezo wa kuisaidia Simba msimu huu licha ya kuwa nyota wapya waliosajiliwa wana viwango vikubwa, nimejipanga vizuri kuhakikikisha narejea kikosini.


"Majeraha ya goti ndiyo yamenirudisha nyuma lakini sasa nimepona na nitapigania kurejea kikosini katika mzungumko wa pili licha ya kuwa na changamoto toka kwa nyota wapya wazuri waliosajiliwa kutokana na umahiri wao," alisema Awadh.

Mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar alisema mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu hivyo kwa mujibu wa kanuni anaruhusiwa kufanya mazungumzo na timu nyingine itakayohitaji huduma yake. 

Kanuni za usajili zinamruhusu mchezaji kuzungumza na timu nyingine kwa ajili ya makubaliano ya usajili mpya akibakiza miezi sita.

Post a Comment

 
Top