BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Azam, Nassor Idrissa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa timu hiyo akichukua nafasi ya Marehemu Alhaji Said Mohamed Abeid, aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwezi huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba iliyotumwa kwa vyombo vya habari pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwafahamisha mabadiliko hayo huku Shani Christoms Mligo akichukuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti iliyokuwa inaogozwa na Idrissa.

Mabadiliko hayo ya kiuongozi yamefanywa na Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC, ambapo uteuzi huo umeanza rasmi leo Novemba 29.

Post a Comment

 
Top