BOIPLUS SPORTS BLOG

BARCELONA, Hispania
RAIS wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu anaamini mshambuliaji wao nyota raia wa Argentina Lionel Messi atasaini mkataba mpya utakaomweka kwa Wakatalunya hao hadi mwisho wa maisha yake ya soka.

Mkataba wa nyota huyo unamalizika mwaka 2018 ambapo makubaliano ya kuongeza kandarasi mpya bado hayajafikiwa lakini Rais huyo anaamini Messi hataikacha timu hiyo.

Kulikuwa na tetesi kuwa mchezaji huyo bora wa dunia mara tano atajiunga na Kocha wake wa zamani Pep Guardiola anayeifundisha Manchester City baada ya kumaliza mkataba wake.

Bartomeu alisema "Messi ni mchezaji mwenye kipaji cha ajabu anapendwa na kila mtu hapa na sisi kama viongozi tutajitahidi kuhakikisha anabaki kwa muda mrefu zaidi," alisema Rais huyo wakati akitambulisha udhamini mpya wa klabu hiyo.

Post a Comment

 
Top