BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
Mzee Said Mohamed

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Klabu ya Azam FC, Said Mohammed ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Azam FC, Saady Kawemba kwamba marehemu ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF amepatwa na umauti  huo akiwa anaendelea na matibabu hospitalini hapo.

Mohamed alikuwa meneja mkuu wa kampuni ya Said Salim Bakhresa kabla hajastaafu na kwenda kuiongoza Azam FC.

Habari zaidi tutawaletea hapa hapa BOIPLUS

Post a Comment

 
Top