BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
BEKI wa Simba Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' tayari amesaini mkataba wa miaka miwili leo wenye thamani ya Sh 40 milioni.

Beki huyo amesaini mkataba huo baada ya kufanyika makubaliano ya awali yaliyofanyika wiki iliyopita chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe ambapo leo mkataba wake ameusaini chini ya Rais wa Simba, Evans Aveva.Kwasasa Zimbwe Jr ni mali halali ya Simba baada ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali huku zingine zikimuhusisha kwenda Yanga.

"Tumemalizana sasa na Simba hivyo Zimbwe ni mali yao Wanasimba kwa miaka miwili, amepewa baraka zote na ninaamini atafanya kazi yake vizuri," alisema Meneja wake Herry Mzozo.

Post a Comment

 
Top