BOIPLUS SPORTS BLOG

DORTMUND, Ujerumani
BORRUSIA Dotmund imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani uliofanyika kwenye uwanja wa Signal Iduna Park huku matokeo hayo yakiwaweka kileleni wageni wa ligi hiyo, RB Leipzig kwa kuwa na pointi 27.

Mshambuliaji raia wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang ndiye aliyepeleka kilio kwa 'Bavarians' dakika ya 11 baada ya kuwazidi ujanja mabeki kabla ya kumfunga kipa Manuel Nuer.

Frank Ribery, Robert Lewandowsky na Thomas Muller walijitahidi kutafuta goli la kusawazisha kwa nguvu lakini vijana wa Thomas Tuchel walikuwa makini zaidi kuhakikisha hawakubali kufungwa.

Bayern wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 24 baada ya kucheza mechi 11 huku Dotmund wao wakifikisha alama 21.

Post a Comment

 
Top