BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
KOCHA Pep Guardiola amekataa kufungwa mara mbili na timu yake ya zamani baada ya kuiongoza Manchester City kuichapa Barcelona mabao 3-1 kwenye mchezo wa marudiano wa ligi ya Mabingwa barani Ulaya uliopigwa Uwanja wa Etihad.

Mchezo iliyopita kwenye Uwanja wa Nou Camp City ililala mabao 4-0 huku Lionel Messi akifunga mabao 3 'hat trick' na Neymar akifunga moja.


Messi ndiye alifunga bao la Barca dakika ya 21 baada ya kupokea pasi maridhawa ya Neymar kabla ya Ilkay Gundogan kusawazisha dakika ya 39.

Kelvin De Bruyne aliipatia City bao la pili dakika 51 kwa mpira wa adhabu aliopiga kando kidogo ya kisanduku cha penalti kabla ya Gundogan tena kupiga msumari wa mwisho dakika ya 74.


City walikuwa na nafasi ya kupata mabao zaidi lakini  washambuliaji wake Sergio Aguero na Rahim Sterling hawakuwa kwenye ubora wao kwani walipata nafasi nyingi ambazo hawakuzitumia.

Matokeo mengine ya mechi za Klabu Bingwa zilizochezwa

Basel 1-2 PSG
Ludogorets 2-3 Arsenal
Bekistas 1-1 Napoli
Benfica 1-0 Dynamo Kyiev
Borussia Moench'bach 1-1 Celtic
Atletico Madrid 2-1 FC Rostov
PSV Eindhoven 1-2 Bayern Munich

Post a Comment

 
Top