BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Simba, Hassan Hassanol amejiuzulu nafasi hiyo.

Kamati hiyo inaongozwa na Musley Al Ruweh ndiyo inayosimamia mipango yote ya timu ikiwemo kuhakikisha inafanya vizuri kwenye mashindano yote ikiwemo ligi kuu.

Habari kutoka ndani ya Simba ambazo pia zilienea kwenye baadhi ya mitandao zinasema kuwa Hassanol amejiuzulu siku chache kabla ya mechi yao ya jana Jumatano dhidi ya Prisons ambapo Simba ilifungwa bao 2-1 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Habari zaidi zinadai kuwa Hassanol ameamua kuachia ngazi ili kuwapa nafasi  wajumbe wenzake huku ikidaiwa kuwa hakukuwepo na mahusiano mazuri ya kiutendaji.

Hata hivyo, Hassanol amesema kuwa, "Tupo pamoja kuendesha Simba naamini kila mmoja ana mchango wake wa kuisadia Simba, nimeamua nipumzike kidogo. Naamini waliopo watafanyakazi nzuri,".

Hassanol ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Simba miaka ya nyuma hakuweza kufafanua zaidi sababu za yeye kukaa pembeni.

Post a Comment

 
Top