BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
Jesse Were kulia akiwa na meneja wake George 'Mendez' Bwana (katikati)

BAADA ya Jesse Were kutamka kuwa hawezi kuja kucheza nchini kutokana na wakenya wengi kutopata mafanikio wakiwa hapa, imefahamika kuwa sababu kubwa ni ofa alizopokea kutoka klabu nne tajiri barani Afrika ambazo zinapambana na Yanga kupata saini yake.

Klabu hizo ni TP Mazembe ya DR Congo, Al Ahly ya Misri, Free States na Ajax Capetown zote za Afrika Kusini. Klabu hizo nne ni miongoni mwa klabu bora Afrika na zenye utajiri mkubwa kuliko Yanga.


TP Mazembe

Straika huyo wa Zesco United  anayefahamiana vizuri na kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina aliyekuwa kocha wa mabingwa hao wa Zambia hajaonyesha nia ya kutua Yanga kwa kile alichodai hafurahishwi na mambo yaliyowahi kuwatokea wachezaji wenzake walipokuja kucheza soka hapa nchini.

BOIPLUS ilizungumza na Meneja wa mchezaji huyo, George 'Mendez' Bwana ili kujuwa mustakhabali wa mteja wake alisema kuwa kwasasa wametulia kwanza mpaka ligi ya Zambia itakapomalizika hivi karibuni huku akiweka wazi kuwa kwa timu yoyote itakayomuhitaji iandae dola 150,000 sawa ni zaidi ya Sh 300 milioni. "Ni kawaida kwa timu kumtamani mchezaji mzuri kama Jesse lakini tutaamua kulingana na hela watakayotoa na mapendekezo ya mchezaji wapi anataka kwenda kucheza atakapokuwa na uhuru napo.

"Yanga wamezungumza nasi ila yote yatafanywa ligi ikimalizika na sio Yanga tu kuna timu kubwa kama TP Mazembe, Ajax, Al Ahly, Free States na zipo tayari kutoa pesa hiyo ila tunasubiri kwanza tufanye mambo kwa umakini na utulivu, kwani Jesse bado hajamaliza mkataba wake na Zesco," alisema George.

Post a Comment

 
Top