BOIPLUS SPORTS BLOG

GRIEZMANN: NILIKUWA NAMTANIA RONALDO SIMCHUKII

MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amesema alikuwa anamtania Cristiano Ronaldo kuwa anamchukia ila anamuheshimu sana na maneno yake juu ya kumchukia ilikuwa kejeli tu baada ya kushindwa kusahau vipigo mfululizo alivyopata kutoka kwa Mreno huyo.

Hivi karibuni Ronaldo aliongelea kuhusu maneno alioambiwa na mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa kuwa anamchukia walipokutana katika jiji la Miami siku chache baada ya kuwafunga 'hat trick' kwenye mechi ya ligi.

Ronaldo na Griezmann wote wapo katika kinyang'anyiro cha kugombania tuzo ya mwanasoka bora wa dunia kwa mwaka 2016 ambapo wote wanapewa nafasi kubwa ya kutwa tuzo hiyo, Griezmann huenda akawa katika hali mbaya kama ataikosa tuzo hiyo na Ronaldo akaitwaa kwa mara ya nne.


PARDEW AJIFAGILIA KUIONGOZA PALACE. 

Kocha Mkuu wa Crystal Palace, Alan Pardew yupo katika presha baada ya klabu yake kupoteza mechi 5 mfululizo katika Ligi Kuu ya Uingereza. Kocha huyo anatambua kua anahitaji kushinda mechi ili kuweza kukinusuru kibarua chake kabla ya bodi kuketi chini na kufanya maamuzi juu ya mustakabali wa kazi yake.

Pardew bado anaamini kuwa yeye ni mtu sahihi wa kuiongoza  Palace pamoja  na matokeo mabaya waliyoyapata siku za karubuni, Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 alisema "Mimi ni mzoefu na nimekuwa katika kipindi kama hiki mara nyingi huu ni msimu wangu wa tisa katika ligi kuu na ningependa kufikisha msimu wa kumi na  Palace,".

Crystal Palace ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi moja zaidi ya timu ambazo zipo kwenye nafasi ya kushuka daraja na leo itashuka dimbani kwenye uwanja Liberty Stadium huko Wales ikikutana na wenyeji Swansea City.

BENITEZ AMUITA STEVEN GERRARD 

Steven Gerrard ametangaza kutandika daluga juzi Alhamis baada ya kuondoka klabu yake ya  La Galaxy iliopo nchini Marekani akimaliza miaka 18 ya mafanikio kisoka, Kocha wa Newcastle Rafa Benitez ana furaha ya kumsaidia Gerrard kujiunga nae katika kujifunza ukocha.

Kiungo huyo amestaafu soka akiwa na umri wa miaka 36 anatazamiwa kua kocha baada ya mwenyewe kukiri kuwa angependa awe kocha baada ya kutundika daruga.

Benitez alisema "Kama anataka aje Newcastle nimuongezee uzoefu wa jinsi ya kufanya vitu na nitampa mawazo. Gerrard ametokea timu ya watoto ya Liverpool sio mbinafsi na alikuwa nahodha na uwanjani na kila alipoongelea timu aliongelea kwa faida".

Gerrard amehusishwa na klabu ya Mk Dons ambayo ilimpa ofa ya kuwa kocha na yeye kuikataa akiamini bila uzoefu asingewezaMalikuwaa.


KLOPP SIJASHTUSHWA NA KIWANGO CHA MATIP.

Baada ya beki Mcameroon, Joel Matip kujiunga na Liverpool kwa uhamisho huru ameweza kufanikiwa kuzoea haraka mazingira ya klabu hiyo na kuisaidia kukwea nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Chelsea katika msimamo wa ligi kuu Uingereza.

Matip ameweza kutengeneza ukuta imara wa Liverpool akishirikiana  na Dejan Lovren ambapo mpaka sasa waneruhusu mabao 14 tu katika mechi 12. Beki huyo mwenye umri wa miaka 25 amejihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha majogoo hao wa Anfield.

Kocha mkuu wa Liverpool, Jurgen Klop alinukuliwa akisema "Ningeshangazwa ingekua na maana kuwa  nilikuwa na mawazo hasi juu yake tulivyomsajili tulijua utayari wake kuja kuisaidia Liverpool, tulitegemea angefanya vizuri hatukumsajili kwasabbabu alikua mchezaji huru,". 

Klopp alisema hayo akitarajia kuwakaribisha Sunderland katika dimba la Anfield.

Post a Comment

 
Top