BOIPLUS SPORTS BLOG

KOCHA mkuu wa timu ya Liverpool mjerumani Jurgen Klopp amesema timu yake inaweza kukabiliana na wapinzani bila ya kuwepo kiungo fundi raia wa Brazil Phillipe Coutinho baada ya nyota huyo  kupata majeraha katika mechi dhidi ya Sunderland wikiendi iliyopita.

Kiungo huyo  alianza vizuri msimu wa 2016/17 kwa kufunga magoli matano katika mechi 13 mpaka sasa lakini Klopp bado anaamini wataibuka na ushindi kwenye mchezo wa Capital One dhidi ya Leeds United katika dimba la Anfield.

Klopp alisema "naweza sema hakuna kisingizio chochote kwa sasa, pamoja na uzuri wa Coutinho ila hawezi badili matokeo peke yake uwanjani ila 
kila mtu anahitaji kupigania  timu".

Coutinho anategemea kuwa nje ya uwanja kwa wiki tano hadi sita.
DEL BOSQUE AMPIGIA CHAPUO SIMEONE
Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Hispania Vicente Del Bosque amempigia chapuo kocha Diego Simeone wa Athletico Madrid kunyakua tuzo ya kocha bora kwa mwaka 2016 tuzo inayotolewa na FIFA.

Del Bosque ambae alistaafu kufundisha soka mwezi Juni alitwaa tuzo hiyo mwaka 2012 huku akiwa mshindi wa pili miaka miwili kabla.

Simeone ameiongoza Atletico kufikia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu nchini Hispania na washindi wa pili katika klabu bingwa barani ulaya msimu uliopita na kumfanya Del Bosque kuamini Muargentina huyo  anastahili tuzo hiyo. 

 Orodha ya makocha wanao wania tuzo hiyo ni Pep Guardiola (Man City) Luis Enrique (Barcelona), Zinedine Zidane(Real Madrid), Claudio Ranieri(Leicester City) na Kocha wa timu ya taifa ya Ureno Fernando Santos.REDKNAPP  ALITAKA KUWASAJILI HAZARD NA SUAREZ SPURS
Aliyekuwa kocha wa timu ya Tottenham Hotspurs Harry Redknapp amesema kiungo mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard na mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez wangekuwa wachezaji wa Spurs kwa sasa kama angefanikiwa kuwasajili.

Kocha huyo amesema Hazard alikuwa na nia ya kujiunga na Spurs huku pia akiwa na mpango wa kumsajili Suarez kwa wakati ule alipokuwa akikinoa kikosi cha Spurs kilichomaliza msimu wa mwaka 2011/12 kikiwa nafasi ya nne.

Redknapp alisema "nilipokua naiongoza Tottenham nilifikiria kuchukua ubingwa wa ligi kuu na niliamini hilo, tuliwapata Ryan Nelsen na Louis Saha kwa uhamisho huru tulikua na majeruhi katika beki ya kati na mshambuliaji na kama tungeweza  kuwasajili  Suarez na  Hazard au mmoja kati yao basi tungekuwa kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa".

Post a Comment

 
Top