BOIPLUS SPORTS BLOG

MOURINHO ASEMA LIGI BADO MBICHI

MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho amesema timu yake ipo nyuma kwa pointi 12 dhidi ya vinara Chelsea ila hawajakata tamaa ya ubingwa kwavile msimu bado haujaisha alipokuwa akizungumzia mchezo wa leo dhidi ya West Ham United.

Mourinho alisema  "Msimu huu ligi ni ngumu timu zimejiandaa vizuri lakini pointi tatu ni muhimu kwetu kwenye mchezo wetu dhidi ya West Ham".

United ina pointi 19 ikiwa nafasi ya sita baada ya kushuka dimbani mara 12 na endapo itapoteza mchezo wa leo na Everton pamoja na Watford wakashinda mechi zao Mashetani hao watatupwa hadi nafasi ya katika msimamo.ENRIQUE  ANATAKA USHINDI TU REKODI BAADAE

Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema kuelekea mchezo wao dhidi ya Real Sociedad katika dimba la Anoeta ambalo ni gumu sana kwao kutoka na pointi tatu hawataangalia rekodi za nyuma bali ni kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mtanange huo.

Kocha huyo alisema "Siangalii yaliopita kikubwa ni kuangalia jinsi gani tunaweza kuibuka na ushindi kama ilivyokuwa  dhidi ya Celtic mahali ambapo ni pagumu kushinda"

 Barcelona imekutana na Sociedad katika   dimba hilo mara saba ikiwa mara sita katika ligi na mara moja katika kombe la mfalme na ikiwa haijashinda mchezo hata mmoja tangu mwaka 2007 ambapo Barca watatakiwa washinde ili kupunguza idadi ya pointi saba dhidi ya vinara Real Madrid.

Post a Comment

 
Top