BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
MCHEZAJI Langa Lesse Bercy wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 aliyekatiwa rufaa na Tanzania kutokana na madai ya kuzidi umri ameshindwa kutokea kwenye vipimo vya mifupa vilivyokuwa vifanyike jijini Cairo Misri asubuhi ya leo kwa sababu ya eneo analoishi kuiripotiwa kuwa na vita.

Ujumbe wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) uliwasili jijini humo toka Novemba 17 kwa ajili ya zoezi hilo ambalo lilikuwa lifanyike saa 5:00 kwa saa za Misri.

Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas ameithibitishi BOIPLUS kuwa mchezaji huyo hakutokea kwenye vipimo kutokana na sababu hizo ambazo hawana uhakika kama ni za kweli kwakua hawajapata taarifa zozote za kutokea vita nchini Congo.

"Hizo taarifa ni za kweli mchezaji Langa Bercy ambaye tulimkatia rufaa ameshindwa kutokea kwenye vipimo hii leo lakini tunapaswa kuendelea kuwa watulivu mpaka suala hili litakapopatiwa ufumbuzi," alisema Lucas.

TFF wamelipia gharama zote za vipimo na za watu wote watakaohusika lakini mpaka sasa haijafahamika kama watarudishiwa pesa zao kutokana na zoezi hilo kutofanyika au la.

Post a Comment

 
Top