BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu
RAIS mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ameyafunga mashindano ya NBA Junior yaliyoshirikisha vijana wa umri wa miaka 14 kutoka shule mbalimbali za msingi yaliyokuwa yanafanyika  katika viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park, jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika hapa Tanzania yalianza mwezi Aprili huku muamuko mkubwa ukionekana kwa vijana walikokuwa wakishiriki katika mchezo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rais Kikwete ambaye ni mpenzi mkubwa wa Kikapu alisema Tanzania ni nchi iliyojaliwa vipaji ambavyo vikifanyiwa muendelezo siku za mbeleni tutakuwa bora zaidi Kimataifa. 

"Michezo huwasaidia vijana kuimarisha afya pia  kutojihusisha na vitendo viovu ambavyo vinaweza kuharibu mustakabali mzima wa maisha yao ya baadaye,"alisema Kikwete.

Rais Kikwete alisema Kiwanja hicho kimekuwa na msaada mkubwa kwa vijana kujifunza kikapu ambapo hadi sasa zaidi ya watu 50,000 wanahudhuria kufanya mafunzo ya mchezo huo. 


Katika fainali hiyo Orando Magic waliibuka na ushindi wa pointi 21 - 18  dhidi Tusiime .

Post a Comment

 
Top