BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
KOCHA Mkuu wa Mbeya City, Kinnah Phiri amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wao wa jana Jumatano dhidi ya Yanga nakuchagiza ushindi wa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mashabiki wa Mbeya City walijitokeza kuishangilia timu yao ili kuwapa hamasa Wachezaji ambao waliona wana deni kulipwa kwa mashabiki wao katika dimba lao la nyumbani. Ushindi huo kwa City ulikuwa ni wa kwanza kuwafunga Yanga tangu wapande ligi kuu.

"Hakika ilikuwa siku nzuri mashabiki walijitokeza kwa wingi sana na walikuwa wakishangilia kwa nguvu kubwa hali iliyoongeza nguvu kwa wachezaji hadi kuibuka na ushindi," alisema Phiri.
Wachezaji wa Mbeya City wakienda kushangilia bao na mashabiki wao

Phiri alisema ilibidi abadili mfumo ili kuweza kuwazuia Yanga ambao wamekuwa wakitumia sana winga kuanzisha mashambulizi na kuwaagiza viungo wake kuhakikisha wanadhibiti mianya yote hasa Simon Msuva aliyeonekana kuleta madhara langoni mwao.

Mabao ya City yalifungwa na beki Hassan Mwasapili na Kenny Ally huku bao la Yanga likifungwa na Donald Ngoma. City ambayo imefikisha pointi 19 kesho Ijumaa wataanza safari ya kuelekea Morogoro kuwafuata Mtibwa Sugar, mechi itakayochezwa Uwanja wa Manungu.

Post a Comment

 
Top