BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
UZINDUZI wa michuano ya Kombe la FA 2016 zitafanyika jijini Tanga kuanzia Novemba 19 katika Uwanja wa CCM Mkwakwani kwa mchezo kati ya Muheza United dhidi ya Sifa Politan ya Temeke.

Msimu huu michuano hiyo itashirikisha timu 84 ambapo mabingwa wa mikoa pia watashiriki tofauti na mwaka jana ambapo timu 64 pekee kabla ya Yanga kuibuka Bingwa kwa kuichapa Azam mabao 3-1.

Bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo mwakani timu ya Azam FC itashiriki baada ya kupoteza kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Yanga ambao watacheza ligi ya Mabingwa Afrika.

Michuano hiyo pia itaonyeshwa moja kwa moja  na kituo cha Luninga cha Azam TV ambao ndiyo wadhamini wakuu kwa miaka mitano kutokana na mkataba ulioingiwa na Shirikisho la  Mpira wa miguu (TFF).

Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas alisema ni matarajio ya Shirikisho hilo kuona ligi yenye ushindani baada ya timu kuongezeka kulinganisha na mwaka uliopita.

"Ligi itazinduliwa Novemba 19 kule Mkwakwani jijini Tanga kati ya Muheza United na Sifa Politan na mwaka huu timu zimeongezeka tofauti na mwaka jana ambapo tunatarajia ushindani mkubwa," alisema Lucas.

Post a Comment

 
Top