BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
 Balozi wa Sweden nchini Katharina Rangnitt (kulia)

KATIBU mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja amefunga kozi ya makocha wanawake ya siku 10 iliyoshirikisha washiriki 27 wakiwa ni walimu toka vyuo mbalimbali vya maendeleo ya jamii nchini chini ya Mkufunzi Wilfred Kidao.

Kiganja amelitaka Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuwabana wahitimu hao kwenda kufundisha soka katika maeneo yao na sio kufungia vyeti ndani na elimu waliyoipata ikawa kazi bure ili kuinua soka la Wanawake nchini.

"Lazima TFF muweke utaratibu ambao utawabana wahitimu  wanaopata mafunzo ya kozi mbalimbali kuhakikisha wanatumia elimu wanayoipata kwa manufaa ya jamii inayowazunguka la sivyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu," alisema Kiganja.


Kwa upande wake Balozi wa Sweden nchini Katharina Rangnitt ambaye alikuwa mgeni mwalika aliipongeza TFF kwa kutoa kozi hiyo kwa Wanawake kutokana na kuthamini mchango wao ambao umekuwa ukipanda kwa kasi kila kukicha.

Nae Katibu mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa alisema kwa sasa timu ya Taifa ya Wanaweza ya Tanzania 'Twiga Stars' imekuwa ikiitangaza vizuri Tanzania barani Afrika ambapo mwaka jana ilikuwa miongoni mwa timu nane bora licha ya kushindwa kufuzu fainali za AFCON.

"Twiga Stars sasa inaogopwa Afrika na jitihada hizi tunazifanya ili kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri Kimataifa" alisema Mwesigwa.

Post a Comment

 
Top