BOIPLUS SPORTS BLOG

SOUTHAMPTON, Uingereza
LIVERPOOL imeshindwa kuongeza pointi tatu kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza baada ya kulazimishwa sare tasa na Southampton mchezo uliofanyika St Mary's.

Liverpool imeendelea kukaa kileleni mwa msimamo baada ya kujikusanyia alama 27 sawa na Manchester City wakitofautiana  mabao ya kufunga na kufungwa huku Chelsea wakishika nafasi ya tatu wakiwa na alama 26 ambao kesho watashuka dimbani kucheza na Middlesbrough.

Golikipa Freiser Foster ndiye aliyewanyima wenyeji pointi tatu baada ya kuokoa michomo mikali ya akina Sadio Mane, Phillipe Coutinho na Robert Filmino ambao walikuwa wakishambulia kwa muda mwingi wa mchezo.

Vijana wa Kocha Jurgen Kloop walifanya kila jitihada kuhakikisha wanaondoka na alama zote ugenini lakini pia wenyeji wanaonolewa na Manue Puel walikuwa makini zaidi.


Katika mchezo mwingine kiungo Yaya Toure ameisaidia Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 baada ya kufunga yote mawili katika mechi yake ya kwanza ya ligi tangu Kocha Pep Guardiola kupewa kibarua cha kukinoa kikosi hicho dhidi ya Crystal Palace ugenini.

Mechi nyingine zilizochezwa leo
Man United 1-1 Arsenal
Everton 1-1 Swansea City
Stoke City 0-1 Bournemouth
Sunderland 3-0 Hull City
Watford  2-1 Leicester City.

Post a Comment

 
Top