BOIPLUS SPORTS BLOG

NDOLA, Zambia
UONGOZI wa Klabu ya Zesco United ya Zambia umetangaza mapema asubuhi ya leo kuwa Kocha wao mkuu George Lwandamina amejiuzulu nafasi hiyo kuanzia sasa.

Zesco imekubali kujiuzulu huko na wamemtakia kila la kheri huko aendako na wanaheshimu mchango wake mkubwa kwa timu hiyo kwa muda wote waliokuwa nae.

Lwandamina alijiunga na miamba hiyo ya Zambia mwaka 2014 na kuiongoza kushinda kombe la ligi mara mbili, Kombe la Benki ya Barclays, Ngao ya Jamii pamoja na kuifikisha hatua ya nusu fainali ya Klabu Bingwa barani Afrika mwaka huu.

Mtendaji mkuu wa Klabu hiyo Justin Mumba alisema kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya Kocha msaidizi Tenant Chembo mpaka mwisho wa msimu kabla ya utaratibu mwingine kufuatwa hapo baadae.

Taarifa ambazo BOIPLUS imezipata kuwa Lwandamina atatua nchini keshokutwa Jumatano tayari kujiunga na Mabingwa watetezi wa ligi kuu timu ya Yanga akiwa Kocha Mkuu na ataanza kibarua chake mzunguko wa pili wa ligi ya Vodacom.

Post a Comment

 
Top