BOIPLUS SPORTS BLOG

George Lwandamina

Karim Boimanda, Dar
KOCHA wa zamani wa Zesco United aliyevunja mkataba na wababe hao wa Zambia, George Lwandamina ametua nchini saa saba usiku wa kuamkia leo tayari kuanza kazi ya kuwanoa watoto wa Jangwani, Yanga.

Yanga wanashuka katika dimba la taifa kesho Alhamis kuvaana na Ruvu Shooting ukiwa ni mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom huku ikidaiwa kuwa hiyo ni mechi ya mwisho kwa kocha Hans Van Pluijm.

Taarifa zilizopo ni kwamba Lwandamina amesaini mkataba wa miaka mitatu na Yanga huku akitarajia kulipwa mshahara wa Dola 18,000 ambao ni mara sita ya ule aliokuwa akipokea alipokuwa anaifundisha Zesco.

Lwandamina atakuwepo uwanjani kesho akishuhudia kazi ya Pluijm aliyeipa ubingwa Yanga misimu miwili mfululizo.

Post a Comment

 
Top