BOIPLUS SPORTS BLOG

Mpigapicha Wetu
 Picha hizi tatu za juu zinaonyesha mandhari ya uwanja wa Taifa wa Congo Brazaville unaotambulika kama 'Kintele Complex' ambao ili kuufikia unalazimika kupita juu ya daraja lenye urefu wa takribani kilomita saba


 Nje ya uwanja mkuu kuna viwanja vingine viwili vya mazoezi na mechi ndogo, vipo katika hali ya ubora huku vikipewa matunzo ya hali ya juu. Kimoja ni cha nyasi bandia na kingine cha nyasi za asili. Pamoja navyo, kuna viwanja vya michezo mingine


Hili ni bwawa kubwa kwa ajili ya kufanyia mazoezi ya kuogelea Ukiwa ndani ya himaya hiyo pia utakutana na bwawa jingine kwa ajili ya mashindano ya kuogelea. Bwawa hili liko ndani ya uwanja na watazamaji hulipia kiingilio kwenda kutazama michuano yoyote inayoendelea
Wageni wanaofika katika uwanja huo hawana haja ya kwenda mbali kutafuta makazi, uwanja huo una hoteli kubwa ya kisasa na yenye hadhi ya juu ambayo pia ina ukumbi unaoweza kuhudumia watu zaidi ya 500 kwa huduma zote ikiwemo chakula

 Timu kadhaa zimealikwa kwenye michuano maalum inayofanyika nchini humu, kila klabu imepewa basi maalumu la kutembelea. Jumla ya mabasi makubwa 30 yapo tayari kwa ajili ya timu za michezo mbalimbali

 Hili ndilo basi walilopewa APR ya nchini Rwanda mara baada ya kuwasili kwa ajili ya mashindano maalumu yanayohusisha timu  nne za Congo na mbili za nje


 Mabasi madogo aina ya Toyota Coaster  pia yapo 20 kwa ajili ya vikosi vidogo na viongozi Pia kuna magari mapya madogo ambayo hutumika katika kubeba viongozi


Muonekano wa ndani ya uwanjani uwanja uko hivi. Uwanja huu una uwezo wa kuingiza watazamaji 68,000 ambao ni 8,000 zaidi ya wanaoingia katika uwanja mkuu wa Taifa nchini Tanzania. Kintele umeezekwa pande zote hivyo hakuna mtazamaji anayepigwa na jua wala mvua.

Post a Comment

 
Top