BOIPLUS SPORTS BLOG

MADRID, Hispania
WACHEZAJI wa timu ya Real Madrid jana walivaa jezi zilizotengezezwa kwa kutumia chupa za maji zilizotupwa bahari ya Hindi katika mchezo walioibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sporting Gijon katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Real Madrid walivaa jezi hizo zilizotengenezwa na wadhamini wao Adidas ikiwa ni kampeni ya kuweka safi bahari ya Hindi ambapo jezi moja ilihitaji chupa 28 kukamilisha utengenezwaji huo huku kikosi kizima kilichoanza kikitumia chupa 308. Kwenye shingo ya jezi kwa ndani kuliandikwa "kwa ajili ya bahari" huku jina la wadhamini likiandikwa kwa wino mwepesi na ikionyesha kwa ndani baada ya kuloa na hii ni baada ya mvua kunyesha.

Adidas wametengeneza jezi hizo zikitumika pia na Bayern Munich ya Ujerumani huku bidhaa mbalimbali zikianza kutengenezwa kutokana na chupa hizo vikiwemo vitu vya ndani ya gari, bidhaa za umeme na nguo za michezo.

Katika mchezo huo mabao yote ya Madrid yalifungwa na Cristano Ronaldo.

Post a Comment

 
Top