BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
MAJIMAJI FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Mwadui FC mtanange uliopigwa kwenye Uwanja wa Mwadui Complex.

Mfanyeje Yusuph ndiye aliyepeleka kilio kwa Wachimba madini hao dakika ya 93 kwa kichwa akimalizia mpira wa kona huku beki David Luhende akishindwa kuokoa hatari hiyo.

Mwadui walitengeneza nafasi kadhaa pamoja na Wanalizombe lakini umakini wa safu zote za ushambuliaji ulipelekea mchezo huo kukamilika kwa wenyeji kulala kwa bao hilo moja pekee.

Tangu kurejea kwa Kocha Kali Ongala Majimaji imekuwa ikipata matokeo huku morali ya Wachezaji ikipanda na moyo wa kupambana ikionekana kurudi kwa kasi hali ambayo haikuwepo mwanzoni wakati ligi imeanza.

Wanalizombe wamemaliza mzunguko wa kwanza wakiwa na pointi 16 wakiondoka chini kwenye timu tatu za mwisho zinazoshika mkia.

Mchezo mwingine Mtibwa Sugar imeifunga Mbeya City bao 1-0 lililofungwa na Haruna Chanongo na kuwapandisha hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 23.

Post a Comment

 
Top