BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
MASHETANI wekundu Manchester United leo wameshindwa kuutumia vema uwanja wao wa nyumbani, Old Trafford baada ya kulazimishwa sare ya bao moja katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Arsenal.

Wenyeji ambao walizidiwa kwa kiasi kikubwa na washika bunduki hao wa Emirates walikuwa wa kwanza kupata bao lililowekwa nyavuni na Mhispania Juan Mata katika dakika ya 68 akimaliza pasi nzuri ya Ander Herrera aliyeingiza ndani mpira wa pasi fupi ya Paul Pogba.

Kocha Arsene Wenger alimtoa Carl Jekinson dakika ya 84 na kumuingiza Alex Oxlade Chamberlain aliyefanya maajabu kwa kupiga krosi kali iliyotua kichwani mwa Olivier Giroud na kuiandikia bao la kusawazisha Arsenal dakika 89.

Matokeo ya mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki 75,000 yameifanya Arsenal ifikishe pointi 25 sawa na Manchester City na Chelsea huku United ikibaki katika nafasi ya sita kwa alama 19 walizojikusanyia. Liverpool wanaocheza na Southampton jioni hii wanaongoza kwa pointi 26.

Post a Comment

 
Top