BOIPLUS SPORTS BLOG

Laudit Mavugo (9) akikabwa na beki wa zamani wa Simba Emery Nimubona kwenye mazoezi ya Vital'O

KAMA ulidhani katika mapumziko mafupi ya ligi kuu wachezaji wote na makocha wamelala basi umejidanganya, straika wa Simba Laudit Mavugo alipanda ndege fasta kwenda kwao Burundi lakini anachokifanya huko ni tofauti kabisa na matarajio ya wengi.

Mavugo aliyetupia mabao manne hadi sasa katika ligi kuu amewasikiliza mashabiki wanaombeza kuwa ni mchezaji wa kawaida sana kisha akaamua kuyafuata mabao yake aliyoyaacha kwenye timu yake ya zamani, Vital'O.

Mara baada ya kuwasili kwao, Mavugo alienda kwa mabosi wake hao wa zamani na kuwaambia "Sijaja kumpumzika, nipeni nafasi nijifue wakanishangae."BOIPLUS iliwahi kufanya mazungumzo na Cedrick Mavugo ambaye ni mdogo wa Laudit na akasema dawa ya ukame wa mabao alionao kaka yake ipo nyumbani kwao Burundi huku akimsihi arejee mara atakapopata likizo. 

Post a Comment

 
Top