BOIPLUS SPORTS BLOG

LUBUMBASHI, DR Congo
TIMU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetawazwa kuwa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga mabao 4-1 Mo Bejaia katika Fainali ya pili iliyofanyika kwenye Uwanja wa Stade TP Mazembe wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 18,000.

Katika Fainali ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 nchini Algeria lakini katika mtanange huu wa pili Waarabu walikubali kubugizwa idadi hiyo kubwa ya mabao.

Mabao ya Mazembe yaliwekwa kimiani na Merville Bope,Rainford Kalaba aliyefunga mawili na Jonathan Bolingi ambao walikuwa mwiba mkali kwa safu ya ulinzi ya Bejaia.

Kalaba ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kufunga mabao 8 huku Bolingi akifuatia kutokana na kucheka na nyavu mara 5.

Timu zote zilikuwa kundi A kwenye hatua ya Makundi sambamba na Yanga ya Tanzania na Medeama ya Ghana ambazo zilitolewa katika hatua za awali.

Post a Comment

 
Top