BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
HUYU Mkubwa Fella ni noma, baada ya kuwawezesha TMK Wanaume Family na Yamoto Band kutisha kwenye muziki wa kizazi kipya 'Bongo Flava', sasa Said Fella ameibuka na bendi ya muziki wa taarabu inayofahamika kwa jina la 'TMK Morden Taarab'. 

Akizungumza na mwandishi wetu, Fella ambaye ndiye Mkurugenzi wa bendi hiyo alisema kuwa  utambulisho wa nyimbo zao mbili za mwanzo utafanyika Novemba 10 kwa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kuanza kupiga nyimbo hizo katika vituo vya radio hapa nchini.

Alizitaja nyimbo mbili ambazo zimesharekodiwa kuwa ni zilizoimbwa na wanamuziki mahiri Mwanahawa Ali aliyeimba wimbo wa 'Sina Pema' na Aisha Vuvuzela aliyeimba 'Kibaya kina Wenyewe' .Bendi hiyo inaundwa na nyota wa muziki wa taarabu ambao ni Mussa Mauji, Mussa Mipango, Omar Tego, Fatuma Nyoro, Mauwa Tego, Babu Kijiko huku wengine waliopo kwenye bendi hiyo wanatoka kwenye kituo cha Mkubwa na wanawe ambao ni Mwanadada Jeza, Hassan Dogo na Ibrahim.

"Hata hivyo tutaendelea kurekodi nyimbo nyingine na kuzitambulisha kama mwendelezo mpaka kufikia siku ya uzinduzi wa albamu na bendi hii," alimaliza Fella.

Post a Comment

 
Top