BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
MSHAMBULIAJI mkongwe wa timu ya Kagera Sugar Danny Mrwanda amewashangaa wachezaji wengi vijana kushindwa kujituma uwanjani hadi kufikia kuwekwa benchi na wakongwe akiwemo yeye.

Mrwanda aliyewahi kuzitumikia timu za Simba na Yanga kwa nyakati tofauti ameiambia BOIPLUS kuwa wachezaji vijana wamekuwa wakilewa sifa mapema kiasi cha kuwahi potea mapema katika medani ya soka.

Mrwanda kushoto akizungumza na mwandishi wa BOIPLUS nyumbani kwake

Mshambuliaji huyo pia alisema kwa sasa Kocha Meck Mexime anampa nafasi ya kucheza dakika 90 ukilinganisha na umri wake huku vijana wakiwa benchi tena hawana wasi wasi na kujiona tayari wamefanikisha kila kitu kwenye mpira hali ambayo itawapelekea kuondoka mapema kwenye soka la ushindani.

"Hata nilivyokuwa Yanga nilikuwa nawaona vijana wanashindwa kujituma na kupambana kupigania namba hali iliyowapelekea kujikuta wanakaa benchi huku vipaji vyao vikipotea taratibu bila kujijua," alisema Mrwanda katikq mahojiano maalum na mtandao huu.

Mrwanda (7) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia Kagera bao

Pamoja na umri wake kuwa mkubwa Mrwanda bado amekuwa na uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza ambapo msimu uliopita alikuwa akichezea Majimaji ya Songea chini ya Kocha Kali Ongala.

Mshambuliaji huyo amewashauri nyota wanaochipukia kwa sasa kujitambua na wakubali kusikiliza ushauri kutoka kwa waliowatangulia ili kuendelea kuwa bora uwanjani pamoja na kujiongezea kipato kwakua soka ni ajira.

Post a Comment

 
Top