BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
DANNY Mrwanda ni miongoni mwa wachezaji wachache waliocheza ligi kuu ya Tanzania kwa muda mrefu huku wakiendelea kukipiga hadi sasa na kuwapa changamoto vijana wanaochipukia. Mrwanda anayeichezea Kagera Sugar alisajiliwa na Simba mwaka 2005 akitokea AFC ya Arusha akiwa bado kijana mdogo.

Wengine ambao wameanza soka kitambo hadi sasa wapo dimbani ni winga wa Majimaji Yusuph Mgwao na kiungo fundi wa Ruvu Shooting Shaban Kisiga ambao wote kwa nyakati tofauti wamewahi kuichezea timu ya Simba. Mbali na kuchezea timu mbalimbali za hapa nchini lakini Mrwanda amewahi kukipiga Al Tadhamon ya Kuwait mwaka 2008-2010, na Dong - Tam, Donoung na Tanhour zote za Vietnam.

BOIPLUS ilifunga safari hadi nyumbani kwa mshambuliaji huyo maeneo ya Kimara Bonyokwa ili kuijua safari yake ya soka hadi kufikia alipo sasa.BABA MZAZI AMPELEKA SIMBA
Mwaka 2005 wakati Mrwanda akichezea AFC Arusha alipata ofa mbili kutoka kwa Simba na Yanga lakini marehemu baba yake alimwambia akasaini kwa Wekundu hao na kuwapiga chini vijana wa Jangwani kwa sababu ambazo hakuziweka wazi.

AFUNGUKA KUHUSU 'ISHU' YA CASILLAS NA MWENZAKE
Mrwanda hakubaliani na adhabu ya kufungiwa miaka miwili golikipa Hussein Shariff 'Casillas' na beki Eric Kyaruzi kwa kutuhumiwa kuhujuma timu yao ya Kagera baada ya kukubali kichapo cha mabao 6-0 dhidi ya Yanga nyumbani. 

"Timu nzima ilichoka kutokana na kusafiri muda mrefu bila kupumzika na pia tulikosa muda wa kufanya mazoezi ndiyo chanzo cha kupokea kipigo kile, wachezaji wale walitolewa kafara tu".
Mrwanda kulia alipokuwa akiichezea Majimaji ya Songea

LIGI HII NI NGUMU KULIKO ZOTE NILIZOWAHI KUCHEZA HAPA BONGO
Mshambuliaji huyo amesimulia mzunguko wa kwanza wa ligi uliomalizika wiki mbili zilizopita kuwa ulikuwa ni mgumu kuliko zote alizowahi kushiriki kutokana na ushindani mkubwa ambapo timu yoyote inaweza kupata ushindi. 

"Simba hawakuwa wamefungwa lakini African Lyon waliwafunga na hakuna mtu aliyeamini kutokana na Wekundu hao kuwa kwenye ubora mkubwa".YANGA, SIMBA CHAMTOTO KWA LIPULI
Licha ya kucheza timu kubwa za Simba na Yanga lakini timu ya Lipuli inayoshiriki ligi daraja la kwanza ndiyo iliyompa pesa ndefu zaidi. Mrwanda ameelezea hiyo ni kutokana na ukweli kwamba alikuwa akilipwa na mtu binafsi japokuwa hajadumu kwa muda mrefu.

"Wakati nipo Lipuli ndiyo nilikuwa nalipwa pesa nyingi sana kulinganisha na sehemu zote japokuwa kulikuwa na wachezaji wengine walikuwa wakilia njaa".Mwamuzi mkongwe Oden Mbaga

ASIMULIA TUKIO LA MWAMUZI ODEN MBAGA
"Kipindi nipo AFC kuna mechi moja ambayo Oden Mbaga alichezesha, nakumbuka ilibaki kidogo nimsababishie kipigo toka kwa mashabiki baada kumdanganya kwa kujiangusha katika harakati za kutafuta ushindi. 

Si unajua mshambuliaji lazima uhakikishe unafunga katika mazingira yoyote ili kuisaidia timu".MAXIMO AMENIFANYA NIJITAMBUE
Mwaka 2006 Kocha raia wa Brazil Marcio Maximo alichaguliwa kukinoa kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars'. Mrwanda anasimulia kuwa kocha huyo ndiye aliyekuwa akimpa ushauri wa kimpira uliomfanya abadilike na kuanza kujitambua mpaka kwenda kucheza soka nchini Asia.NYOSO NI NOMA
Mrwanda alisema katika soka la Bongo hajawahi kukutana na beki katili kama Juma Nyoso aliyemwelezea kuwa ni mlinzi ambaye hana masihara kabisa katika suala la kulinda lango lake, anatumia nguvu nyingi na akili kidogo sana. 

"Mabeki wengi wa sasa ni walaini hakuna kama Nyoso jamaa ni katili kweli kweli".
Mrwanda kushoto akifanya mahojiano na mwandishi wa BOIPLUS

MARUFUKU MTOTO WANGU KUGUSA MPIRA
Mrwanda amejaliwa kupata watoto watatu Prince (8), Precious (4) na Patricia (2) lakini ameweka wazi kuwa hakuna atakayeruhusiwa kucheza soka kwakua kuna changamoto kubwa ambazo amepitia na asingependa wakutanenazo na kwamba urithi pekee atakaowaachia ni elimu.

"Kiukweli hakuna mwanangu atakayecheza soka, mimi niliyopitia yanatosha wao watasoma fani nyingine soka hapana".MAPROO NDIYO CHANZO CHA STARS KUBORONGA
Mrwanda alisema kitendo cha Shirikisho la mpira wa miguu TFF kuruhusu wachezaji wa kigeni saba kucheza ligi ndicho chanzo cha Taifa Stars kuboronga kwakua inalazimishwa wacheze huku wazawa wakikosa nafasi. 

"Wanasajiliwa wachezaji saba wa kigeni kwa bei kubwa halafu hawana viwango lakini kutokana na dau la usajili wanalazimishwa kucheza lazima iathiri timu ya Taifa".


Post a Comment

 
Top