BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
WINGA Simon Msuva anayechezea timu ya Yanga amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Msuva amewashinda nyota wawili kutoka timu ya Simba ambao ni Mzamiru Yassin na Shiza Kichuya ambaye ndiye aliyeibuka mchezaji bora mwezi uliopita.

Katika mwezi Oktoba ambao ulikuwa na raundi sita, Msuva aliisaidia timu yake kupata jumla ya pointi 14 huku akifunga mabao manne, na kutoa pasi tano za mwisho (assist).

Kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Msuva ambaye alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2014/2015 atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Post a Comment

 
Top