BOIPLUS SPORTS BLOG

GENK,Ubelgiji
LICHA ya ukame wa mabao uliomkumba straika Mtanzania Mbwana Samatta, timu ya KRC Genk imeendelea kujikita kileleni mwa kundi F katika michuano ya Kombe la Europa baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi Rapid Wien mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Cristal Arena.

Mshambuliaji Nikos Karelis alifunga bao hilo pekee dakika ya 11 na kuifanya Genk kuongoza kundi hilo baada ya kufikisha pointi 9 sawa na Athletic club Bilbao ambao nao wamewafunga Sasuolo 3-2.

Samatta aliingia dakika ya 84 akitokea benchi kuchukua nafasi ya  Karelis lakini alishindwa kuipatia bao la nyongeza timu yake.

Mchezo mwingine Manchester United iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Feyernood na kuchumpa hadi nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 9 kwenye kundi A ambalo Fenerbache ndiyo vinara wakiwa na pointi 10.

Magoli ya United yalifungwa na Wayne Rooney, Juan Mata na Jesse Lingard huku la nne mlinda mlango Jones akijifunga katika jitihada za kuzuia krosi ya Zlatan Ibrahimovic.

Matokeo ya michezo mengine iliyochezwa  jana;

Fenerbache 2-0 Zorya
FC Astana  2-1 Apoel Nicosia
Olympiacos 1-1 Young Boys
A.Bilbao 3-2 Sasualo
FK Qabala 1-3 Anderlecht
Saint Etienne 0-0 Mainz 05
Zenit 2-0 Maccab Tel Aviv
AS Roma 4-1 Victoria Plizen

Post a Comment

 
Top