BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Mbeya
KOCHA wa Mbeya City, Kinnah Phiri amefurahishwa na ushindi walioupata dhidi ya Yanga lakini ameweka wazi hisia zake kuwa mshambuliaji wale Ditram Nchimbi amemnyima bao la wazi. City imeshinda bao 2-1.

Nchimbi alishindwa kutumia nafasi ya wazi aliyoipata akiwa yeye na kipa wa Yanga Deogratius Munishi 'Dida' ambapo alipiga mpira uliopita nje kidogo ya goli. Mechi hiyo imechezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Phiri ameiambia BOIPLUS kuwa, "Tungeshinda bao tatu leo pengine na zaidi ila Nchimbi kaninyima bao langu la wazi kabisa, pale alitakiwa kumzunguka kipa na kufunga ila sijui aliwaza nini, kikubwa nimefurahi kuvunja mwiko hata Yanga wamekubali kuwa tuliwakamata.

"Mechi ilikuwa na presha kubwa tangu maandalizi yake hata wachezaji wa Yanga kipindi cha pili walianza kucheza rafu sana ili mradi wapate bao, nafurahi nimebaki na pointi tatu na ninakwenda kumalizia ushindi kwa Mtibwa Sugar ili hesabu zangu za kufunga mzunguko wa kwanza na pointi 20 zikamilike," alisema Phiri na kuongeza

"Niliwapa maelekezo wachezaji wangu kwamba watafute ushindi wa haraka maana tayari niliwaona Yanga mechi zao za nyuma kuwa wakicheza dakika kadhaa wanapoteza nguvu, baada ya kupata matokeo niliwataka wacheze kwa kuzuia ili washambuliaji wao wasipate nafasi ya kupita," alisema Phiri.

Yanga imebaki na pointi 27 ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakati Mbeya City wamefikisja pointi 19 na keshokutwa Ijumaa wanatarajia kuanza safari ya kwenda Morogoro kuwafuata Mtibwa mechi itakayochezwa Jumatatu uwanja wa Manungu.

Post a Comment

 
Top