BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Shinyanga
 Jioni ya leo Simba watafanya mazoezi yao ya mwisho katika uwanja wa CCM Kambarage mjini hapa kabla hawajavaana na Stand United hapo kesho

Katika mazoezi ya jana, kamera ya BOIPLUS ilifanikiwa kuwanasa nyota wawili wa timu hiyo, Nahodha Jonas Mkude na Shiza Kichuya ambao mapambano yao uwanjani hapo yalionyesha wazi hawana mchezo, ni kama mechi tu na hakuna aliyeonyesha kumlegezea mwenzake

 Stand United wenyewe waliingia mjini hapa jana mchana wakiwa katika hali ya kujiamini sana huku wakisisitiza kuwa hawajachoka na watapambana kuimaliza Simba. Mitaa ya mji wa Shinyanga imepambwa kwa tambo hasa za mashabiki wa Wapiga Debe hao ambao wamefanikiwa kuzifunga timu za Yanga na Azam katika uwanja huo msimu huu hali inayowapa matumaini ya kuizima Simba pia.


Post a Comment

 
Top