BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Dar
SIMBA haikuwahi kupoteza mchezo wowote tangu ligi ianze, hali hiyo ilipelekea wekundu hao kuchanganyikiwa baada ya bao la dakika za mwisho kabisa lililoipa ushindi wa 1-0 African Lyon

Meneja wa Wekundu hao, Mussa Mgosi alionekana alishindwa hata kukaa chini na badala yake akiishia kuduwaa asiamini kilichotokea

Nahodha Jonas Mkude ambaye amekuwa mhimili mkubwa wa kikosi hicho, alishindwa hata kuinua uso kutokana na simanzi aliyokuwanayo. 

Usingeweza kuwauliza swali lolote Laudit Mavugo, Manyika Peter Jr wala Musa Ndusha halafu upate jibu sahihi. Hapa wanaonekana wakiwa katika mawazo mazitoHuko jukwaani wakati wapenzi na wanachama wengi wakiwa wameshaondoka, kamera ya BOIPLUS ilimnasa Mzee Hassan Dalali akiwa amesalia kwenye kiti asijue kuwa ni muda wa kuondoka uwanjani hapo.

Post a Comment

 
Top