BOIPLUS SPORTS BLOG

MADRID, Hispania
SHUJAA wa Real Madrid Alfredo di Stefano alifanikiwa kufunga mabao 17 dhidi ya Atletico Madrid katika kipindi chake alichoichezea timu hiyo, lakini unajua alichokifanya Cristiano Ronaldo usiku huu?, ni kuivunja rekodi hiyo na kuweka yake baada ya kuwafunga mabao matatu (hattrick) katika mchezo wa La Liga.

Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Vicente Calderon ulikuwa ni wa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini Madrid ndio walifanikiwa kutimiza mipango yao baada ya Ronaldo kufunga bao dakika ya 23 kwa mpira wa adhabu ndogo.Kocha wa Madrid Zinedine Zidane aliwaacha nje mastraika Karim Benzema na Alvaro Morata huku akimtumia Lucas Vazquez aliyekuwa akisaidiwa na Ronaldo pamoja na Gareth Bale mbele ya viungo watatu Isco, Luka Modric na Mateo Kovacic walioonyesha kulimudu vilivyo eneo la kati la uwanja.

Ronaldo alifunga bao la pili dakika 71 kwa penati kabla hajatimiza hattrick yake kwa bao safi la dakika 77 akimaliza kiutulivu krosi ya Bale kutoka upande wa kushoto. Hii ni hattrick ya pili kwa Ronaldo dhidi ya Atletico huku bao hilo likiwa ni la 18 dhidi yao.Kwa ushindi huo Madrid wamefikisha alama 30 wakizidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo huku wakifuatiwa na Barcelona wenye pointi 26.

Post a Comment

 
Top