BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar
MWANAMITINDO ambaye pia  ni mwamuziki wa Bongo Fleva nchini Jokate Mwegelo ameushauri Uongozi wa Klabu ya Yanga kufanya kila kinachowezekana kuhakiksha wanatetea ubingwa wao waliobeba mara mbili mfululizo huku akiyasema hayo kutokana na mwenendo wao usioridhisha.

Jokate ni miongoni mwa wanazi wakubwa wa Mabingwa hao ambapo anaona kama jitihada za makusudi hazitafanyika kuna uwezekano mkubwa wa Ubingwa huo ukaenda kwa watani wao wa jadi timu ya Simba.

Akizungumza na BOIPLUS Jokate alisema kuwa inasikitisha sana kuona timu yake inashindwa kupata matokeo ya ushindi kwenye michezo yao huku watani wao wakiwa kwenye kiwango bora hali ambayo imeanza kuwatisha mashabiki wengi akiwemo mwanamitindo huyo.


"Bado tunayo nafasi ya kutetea ubingwa wetu kikubwa ni viongozi kukaa pamoja na benchi la ufundi kuangalia mapungufu yaliyopo kikosini na sisi mashabiki tuendelee kushikamana itakuwa rahisi kufanya kama ilivyokuwa msimu uliopita," alisema Jokate.

Mbali na soka Jokate pia ni mpenzi wa mpira wa kikapu na alikuwepo katika  viwanja Jakaya Kikwete Youth Park kushuhudia Fainali ya  Mashindano ya NBA Junior yaliyokuwa yakishirikisha wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari walio chini ya umri wa miaka 14 zilizopo jijini Dar es Salaam.

Katika Fainali hizo timu ya Orlando Magic iliibuka Bingwa kwa kuifunga Tusiime kwa pointi 21-18 na kukabidhiwa kikombe pomoja na medali.

Post a Comment

 
Top