BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
Kipre Balou

NYOTA wa Azam FC, Kipre Balou na Jean Mugiraneza 'Migi' wapo njia panda kwenye kikosi hicho baada ya kudaiwa kuwa uongozi wa klabu hiyo hauwezi kuwaongeza mikataba mipya kwani ya sasa inamalizika na tayari kuna mchakato wa nyota saba wa kigeni waliokuja kufanya kajaribio kwamba wanaweza kuchukuwa nafasi zao.

Tayari Azam FC imewapoteza nyota wake wawili, Pascal Wawa aliyejiunga na  El Merreikh ya Sudan pamoja na Kipre Tchetche aliyekwenda Oman na endapo wataachana na hao wawili basi watakuwa na nafasi nne za kujaza kwa wachezaji wa kigeni.

Wachezaji waliopo sasa ukiachana na Migi Pamoja na Balou kuna Fransisco Zekumbawira, Bruce Kangwa, Ya Thomas Gonabo, Daniel Amoah na Enock Atta Agyei.


Jean Babtiste Mugiraneza

Kocha wa Azam, Zeben Hernandez amesema sehemu kubwa anayoifanyia kazi ni safu ya ushambuliaji ambayo imeonekana kutokuwa na makali kama ilivyokuwa msimu uliopita.

"Kuna mapungufu ambayo nimeyaona kwenye mechi zilizopita na nimeyaweka kwenye ripoti yangu, hawa waliopo kufanya majaribio wote nimewaona nitakaoridhika nao watasajiliwa wengine wataachwa," alisema Hernandez.

Azam inajiimarisha ili iweze kuwa na kasi ingawa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 25 lakini bado kiwango chao kilikuwa chini.

Post a Comment

 
Top