BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
KIUNGO wa Simba, Mzamiru Yassin amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa klabu hiyo baada ya kufanya vizuri na kuwasaidia Wekundu hao kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi wakiwa vinara.

Tuzo ya mchezaji bora wa timu ya Simba hutolewa baada kuchaguliwa na wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kupitia mitandao ya kijamii kila mwezi.

Kiungo huyo aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar msimu huu amejihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Kocha Joseph Omog huku akifunga mabao manne katika mzunguko wa kwanza wa ligi wakati timu yake ikiwa na pointi 35 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu.

Omog amekuwa akimwamini Mzamiru na kumpa nafasi ya kucheza karibu mechi zote 15 ambazo Simba wamecheza kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi.

Post a Comment

 
Top