BOIPLUS SPORTS BLOG

LONDON,Uingereza
KWA mara nyingine Tottenham Hotspur imeshindwa kuvunja mwiko wa miaka 26 kupata ushindi kwenye uwanja wa Stamford Bridge baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Chelsea.

Mara ya mwisho kwa Spurs kushinda kwenye uwanja huo ilikuwa Februari 10 mwaka 1990 ambapo ni wachezaji sita pekee waliopo kwenye kikosi hicho walikuwa wamezaliwa.

Kiungo Christian Eriksen aliwapatia wageni bao la uongozi dakika ya 10 kwa shuti kali la mguu wa kushoto nje kidogo ya eneo la hatari lililomshinda golikipa Thibaut Courtois kabla ya Pedro kusawazisha dakika ya 44 akipokea pasi safi ya Nemanja Matic.

Victor Moses aliwapatia Chelsea bao la ushindi dakika 51 baada ya kupokea pasi safi ya Diego Costa upande wa kushoto na kuachia shuti kali lililomgonga Jan Vertonghen na kuingia moja kwa moja wavuni.

Chelsea wamerejea kileleni baada ya kufikisha alama 31 baada ya kushuka dimbani mara 13.

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo

Bunley 1-2 Man City
Hully City 1-1 West Bromwich
Leicester City 2-2 Middlesbrough
Liverpool 2-0 Sunderland
Swansea City 5-4 Crystal Palace.

Post a Comment

 
Top