BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
WAZIRI wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amepokea vifaa vya michezo kutoka kampuni ya Star Times Tanzania kwa ajili ya kuhamasisha na kuvumbua vipaji kuanzia umri mdogo hasa mikoani.

Kampuni hiyo ilimkabidhi mipira 100 na fulana 100 ambazo zitagawanywa maeneo mbalimbali hasa mikoani kulingana na uhitaji wa eneo husika kwakuwa dhamira ni kuhamasisha michezo nchi nzima.

Nape aliishukuru kampuni ya hiyo kwa msaada huo na kuonyesha dhamira ya kuisaidia Serikali kuinua sekta ya michezo nchini huku akiwataka wadau wengine kufuata nyanyo zao kusaidia kwani inahusisha kundi kubwa la vijana ambao itawasaidia kuwaingizia kipato na kupunguza tatizo la ajira.


"Nachukua nafasi hii kuipongeza Star Times Tanzania kwa msaada huu wa vifaa na dhamira ya Serikali ni kuhakikisha michezo inakuwa kila sehemu bila kujali maeneo kwakua nchi hii ni moja," alisema Nape.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Leo alisema wanajitahidi kujitoa kwa kile wanachokipata kuchangia michezo ili kuunga mkono jitihada za Serikali kukuza sekta hiyo ambayo inajumuisha idadi kubwa ya vijana.

"Star Times tumekuwa wadau wakubwa wa michezo hapa nchini na tunaahidi kuendelea na ushirikiano huu na Serikali katika masuala mbali mbali," alisema Leo.

Post a Comment

 
Top